Mpendwa msaikoloji. Sijui nifanye nini. Nimeishi kwenye nyumba yangu ambayo nimepanga kwa kipindi kifupi tu. Naipenda hii sehemu sana kwasababu nyumba ya kwanza wapi niliishi Jyväskylä ilikuwa si mzuri. Kwenye nyumba yangu mpya kuna jirani ambayo amenileta shida tangu mwanzoni. Wakati nilipohama tu nilienda kusalimia yeye na nikapeleka chakula kama zawadi ambayo ni tabia kwenye nchi ninapotoka. Wakati huo tayari aliniangalia kwa ghera na hakuinita kutembelea nyumbani kwake. Sasa ameanza kukonga ukuta na mara chache ameleta karatasi njia ya mlango. Kwenye karatasi imeandikwa mambo ya hasama. Nimeona yeye mara chache na yeye ana angalia mimi kwa ukali. Sijui nifanye nini? Kuna njia kwamba namna gani ya kujitaidi uhusiano na jirani yangu? Lakaba ”tuweze kuendelea vizuri”

Mpendwa lakaba ”Tuweze kuendelea vizuri”. Umekutana na hali ambayo wahamiaji wengi wamepata kuona. Kama kwenye nyumba ya ghorofa hali inatokea wapi watu wanasikia ghera. Watu wanaweza kutoka utamaduni nyingine, labda wanaonekana tofauti na labda wamezoea na tabia tofauti kidogo. Pia watu wanaishi karibu na watu hawezi kuepuka sauti au harufu ya maisha. Kila kitu ambayo ni mpya kwa mtu anasikia kama hataki kushuhulika kabla ya kuona kwamba kitu kipya ni mzuri kuliko kitu cha zamani. Kwa tabia yetu tunapenda mambo ya zamani ambayo tumezoea. Hata mtoto mdogo anatema chakula mwanzoni kabla ya kuzoea. Tunazoea lakini baadaya ya kuonza mara kwa mara vipande vidogo. Baadaye kwenye maisha hii inaendelea vile vile: mbadiliko au kitu ambayo ni kama mgeni inachukua nguvu kuzoea na inahitaji ufanye kazi ili uzoee.

Mtazamo ya wajirani bila sababu ni kitu kigumu mara nyingi kwa wahamiaji. Hasa kwa watu ambayo wamelazimiswa kutoroka kutoka nchi yao ya zamani wanaanza kusikia hali moja ya kusonga. Shauri ambayo ninataka kumpa ni kwamba mwanzoni unaweza kuenda kuongea moja kwa moja kwa jirani kwa utulivu. Kama hufaulu kuongea lugha ya Kifini unaweza kuchukua rafiki ambayo anaongea vizuri. Kitu kimuhimu lakini ni kwamba unaonyesha kwa jirani uko tayari kutatua kitu ambayo yeye anasikia ni shida. Muhimu ni kwamba wewe unaelewa kitu gani imesumbua yeye na unaweza kufanya kitu kwa hali. Kama jirani yako hawezi kueleza kitu cha kurekebisha itakuwa vizuri kupeleka habari kwa bwana wa nyumba. Kwa yeye unaweza kufanya notisi kuhusu kitu kwamba kuna mutu anakusumbua. Hapa Finland ni haramu kusumbua raha ya kuishi kwa mfano kwa njia ya kuingia ndani kwa nguvu, kukataa kutoka, kupiga simu au kutuma ujumbe ambayo yanasumbua. Kama hali ni mbaya unaweza kufanya ripoti kwa polisi pia. Wewe uko na haki na hali hapati ufumbuzi kwa njia ya kunyenyekea. Hakuna mtu ambayo ana haki ya kutedea wewe kwa nguvu na hata hatuwezi kudai kwamba wajirani watakuwa marafiki wetu. Katika utamaduni ya hapa Finland ni kawaida kwamba wajirani hawafahamiani na hata hawasalimiani. Kwa hivyo si ajabu kama jirani ya Mfini amestuka kidoko wakati umeenda kusalimia yeye na kupeleka zawadi. Inawezekana kwamba jirani yako kama Mfini wa kawaida amekuelewa wewe vibaya na kufikiri labda kwamba umesogelea karibu kupita kiasi.

Natoa shauri ya kuenda kushuhulika katika shuhuli za ofisi ya nyumba. Wakati kuna siku ya usafi kwa ghorofa nzima, wakati wa muda wa joto inakaribia au wakati muda wa joto inaisha, uende kuwaona watu na kufurahia kuona wajirani. Pia inawezekana kwamba kwenye chumba cha kilabu cha ghorofa kuna mkutano au sherehe. Wakati wajirani wanapata kujua wewe vizuri na wanakuzoea, wanaanza kufikiri mambo tofauti na hawaogopi wewe tena. Pia katika sehemu unapoishi wana andaa mkutano na pia itakuwa wizuri ukienda pale. Watakuzoea wewe na wanapata kujua wewe polepole. Kitu kimuhimu kwa upande wako ni kwamba unafuata kanuni/sheria/utaratibu ya mwenye nyumba. Inatosha kwamba unaweza kuishi na wengine na raha.

Sirkku Suikkanen msaikoloji

Siirry ylös


 

Яндекс.Метрика