Mpendwa msaikoloji, ninakuuliza Wewe shauri kuhusu shida ya ndoo yangu. Mimi ni mwanamke Kifini na naishi Finland kusini. Nimeolewa kwa kipindi miaka mbili na mwanaume kutoka utamaduni nyingine. Tuko na mtoto wa umri mwaka moja. Tulionana mara ya kwanza wakati nilikuwa likizo kwenye nchi ya bwana wangu miaka nne iliopita. Kujuana na kupenda ilikua kitu kizuri sana. Wakati likizo yangu iliisha nilirudi Finland lakiki muda wote tuliongea kwa njia ya simu. Kisha mwezi moja ya kupita nilirudi na nilibaki kuishi kwenye familia ya bwana wangu. Walinipokea vizuri na nilisaidia kwenye hoteli ambayo ilikuwa mali ya familia. Kazi ya kawaida sikupata lakini bwana wangu alinilisha. Kwasababu tulitaka mtoto wetu apate kusoma vizuri tuliamua kuhama Finland. Hapa Finland wote wawili hatukukuwa na kazi au masomo ya kufanya kwa hivyo mwanzoni ilikuwa shida sana. Hata kama muda imepita mantiki ya maisha hajabadilika sana. Mimi nachunga mtoto nyumbani na bwana wangu hana kazi au jioni ako kwenye hoteli ya pizzeria. Uhusiano yetu sasa imeanza kupata shida kwasababu wote wawili tuko na mawazo mazito kidogo. Mimi nasikia kwamba bwana wangu aweze kusaidia mimi zaidi katika kazi ya nyumbani na kuchunga mtoto. Mimi nafikiri kwamba yeye anatoka nyumbani kwa muda mrefu sana kupita kiasi. Anasema kwamba anaenda kusamilia rafiki yake kumbe anarudi baadaya ya saa sita. Mimi nataka tuweze kuenda kutembelea sehemu pamoja. Mara nyingine marafiki wanafika kututembelea na wanaketi saa nyingi sana wakati mimi naanza kuchoka. Mimi siwezi kuingia mazumgumzo kama mtu mzima na inaonekana kwamba inatocha nikicheka tu au nikisaidia kumwaga chai kwa wageni. Tena mazumgumzo inaanza kwa lugha yao. Mara nyingine nasikia kwamba bwana wangu hafurahii na kitu nilivyo fanya wakati wageni wapo, lakini maelezo mazuri kutoka yeye mimi sipati. Mpigano au mambo kama haya hatuna kwenye uhusiano wetu lakini mimi nasikia kwamba sisi ni wageni. Kwasababu hali ya pesa si mzuri nimesikia mbaya wakati bwana wangu anatuma pesa wetu kwa familia wake wakati wako na shida ya pesa. Hii inaleta vituko. Ni kweli kwamba hata mimi ningetaka susaidia hawa pia lakini hata sisi hatuna pesa ya kunua fanicha mzuri au nguo mpya. Ningependa pia kwasababu muda mrefu imepita kuenda sehemu mzuri kukula chakua kama hoteli mzuri au kuenda kwa kinyozi. Sasa wakati tuna mtoto haiwezekani kuacha uhusiano mara moja. Pia sitaki kwa mtoto wangu familia ambayo imeharibika. Pia mara nyingi nafikiri kwamba hii ni familia namba gani wapi wazazi hawana haki sawa. Lakaba ”Namna gani tuendelee?”
Mpendwa ”Namna gani tuendelee?” Wewe umekuta bwana wako miaka nne iliopita na ndani ya hii mwaka umawahi kufunga ndoo, kupata mtoto na kuhama Finland. Mabadiliko haya yote ni mambo makubwa katika ndani ya muda mfupi na inachukua uzoefu sana. Wewe hukueleza kama Wewe una wajamaa walioweza kusaidia katika maisha ya kila siku na maisha yako ya kuona marafiki yako ilivyo. Kitu cha kwanza ilio kuja kichwani yangu ni kwamba si vizuri kama uko na mtoto wako pekeyako nyumbani na unahitaji kuona marafiki na kupata kuongea labda na wengine walio na mantiki ya maisha kama wewe. Tuseme kwa mfano mafamilia kutoka utamaduni mbali mbali wapi kuna watoto na mama pia. Kuna shirika ulioitwa Mannerheimin lastensjuojeluliitto- shirika la kuchunga haki ya watoto na wizara mfulani wanapanga mkutano kwa wazazi na mkutano wapi watu ambayo wanafanana wanakutana. Mambo kama haya yanaweza kusaidia sana. Uliza sana sana mambo gani inapatikana huku sehemu unapoishi, soma matangazo yote, soma gazeti au tafuta kutoka internet. Unahitaji watu ya kuongea kuhusu maisha ya kila siku na kuhusu mawazo wako. Itakusaidia wewe sana. Inaonekana kwamba bwana wako kwa njia ya kufuata tabia ya utamaduni yake amepata msaidizi na watu wakuongea. Hii ni muhimu sana kwa mandeleo ya roho yake kwasababu anaishi kwenye utamaduni ambayo ni tofauti kabisa amepozaliwa. Pia habari kuhusu uwezo ya kupata kazi kwa kawaida inapatikana njia ya kusikia kutoka rafiki. Msaidizi inapatikana pia katika mambo kubwa kama kuna marafiki. Kuhusu hii kitu ya kutoka nyumbani kwa muda mrefu na kuhusu kufanya nini wakati wageni wamefika kutembelea inabini Nyinyi uongee vizuri kwa pole pole. Inawezekana kwamba hamjui yeye anasubiri nini kutoka wewe au wewe kutoka yeye. Ni muhimu kwamba unaeleza unaposikia kama mwanamke Kifini wakati kumwaga kahawa tu wakati wageni wamefika. Kama bwana wako angekuwa Mfini mambo ingekuwa namna gani? Utoe maelezo na shauri kwa bwana wako na omba yeye atoe shauri kwa wewe. Marafiki, wajamaa na uaminifu kwa hawa ni katika utamaduni mengi kitu kimuhimu sana hata zaidi ya sisi hapa Finland. Wakati mwenzako anahitaji msaidizi watu wako tayari kupunguza muda wao au pesa yao. Kwa hivyo itakuwa vizuri kama utaweza kusoma na kujifunza utamaduni ya bwana wako na upate kujua mambo ya kanisa pia. Mambo kama haya yanasaidia wewe kuona shida gani kimetokea katika shirikiano na wewe na bwana wako. Swali moja muhimu ni kwamba lugha gani unatumia wakati mnaongea. Kama bwana wako hajui bado Kifini vizuri na wewe hujui lugha wa bwana wako inaonekana wote mwaongea lugha ambayo hamjui vizuri? Kupata kujua mtu inachukua muda mrefu. Uzoefu wako kwamba nyinyi ni kama wageni ni kitu ambayo inawezekana kuwa kitu halisi. Hasa kama hakuna lugha moja ya kuongea inaweza kukuwa shida ya kuelewana. Historia ya muda wakati umekuwa pamoja ni pado kipindi kifupi na haiwezekani kwamba mnajuana vizuri. Katika maisha yenu siku za kawaida zimeanza. Kabla ya hii wewe umeishi sehemu ambayo ni ajabu na wapi kila kitu ni mpya bila mawazo mazito ya kila siku. Sasa ni muhimu kwa wote wawili kuanza kukaza kujifunza lugha. Kwa wewe pia ni vizuri kujifunza lugha ya bwana wako kwasababu hii lugha itakuwa lugha moja ya nyumbani kwa mtoto wenu. Kama kuna lugha ya kuelewana italeta nyinyi karibu kama familia. Wakati mantiki ya maisha ni ngumu na kusikia mawazo mazito ni kitu cha kawaida tu. Nitatoa shauri kwamba msichoke na msiache kwaurahisi. Mtengano au mwisho wa shirikiano ni kitu kirahisi kufanya lakini matokeo kwa wote wawili itakuwa kubwa. Siku za kawaida itaingia tu katikia kila shirikiano. Fikiri sasa kwamba kitu gani unapenda na kitu gani unataka kuhusu maisha yako. Hata kama kwa sasa kuna shida familia mwenye utamaduni mbili ni kitu kizuri ni kwa mto kukuwa. Kwa sasa ni muhimu kwamba mnaweza na unapenda kufuata wakati mtoto mdogo anakuwa na anaendelea. Ni maujiza ya bure kabisa furaha kwa nyinyi wawili. Kama inaonekana mantiki haitabadilika uende kuongea ”neuvola” hospitali ya watoto wadogo au upange muda moja kwa moja kwa ”kasvatys ja perheneuvola” hospitali ya familia hapa unapoishi. Huku mnaweza kuenda wote wawili kama familia na mtapokea msaidizi katika hali ya maisha.
Sirkku Suikkanen
msaikoloji