Mpendwa msaikoloji, ninakuuliza wewe kuhusu shida ya ndugu wangu. Yeye haishi hapa Finland wala hawezi kuenda hospitali hivi hivi tu kupata msaidizi. Nimekubali lakini kwa familila wake kwamba nitasaidia na nitatafuta habari. Ndugu wangu haja oa na kwa miaka mingi amesumbuliwa na hali wakati pepo mbaya inaingia. Wakati huo hii pepo mbaya inaweza kuchukua mwili wake na kuanza kuongea na ndomo yake mambo au inaweza kuleta mauvivu ya mvili. Ndugu wangu anahangaika sana, mawazo wake ni mazito na anasikia hakuna tumaini kwa kipindi kirefu. Familia imejaribu kupata msaada kutoka kinyeji ambayo imejaribu kupunga pepo mbaya itoke lakini kwa bado wote wamesema kwamba pepo iko na nguvu nyingi. Hali ya ndugu yangu inasitikisha sana kwasababu yeye tangu mtoto mdogo amepata kuishi maisha nguvu kuliko wenzake. Wakati alikuwa mtoto aliugua sana kwa miaka mingi na halafu mama yake alifariki wakati bado hajaingia shuleni. Baadaya ya hiyo amekuwa na mama wa kambo wawili. Siku hizi wanaangalia hali kutoka upande wa uganga kwenye nchi yangu ya zamani lakini watu wa kawaida bado wanaamini nguvu ya pepo mbaya. Ndugu wangu amesema anajua kwamba pepo mbaya yupo na anakamata sana Mungu na kuomba ili apate nguvu ya kuendelea. Kwasababu kama kitu cha kinyeji hajasaidia jinsi gani tuweze kusaidia ndugu wangu? Lakaba ”Mwenye wasiwasi”.

Mpendwa lakaba ”Mwenye wasiwasi”. Unaeleza hali wapi ndugu wako ako na shida kubwa sana na wapi kupunga pepo mbaya hajaleta msaada. Kama ni vile inabidi kufukiri kama shida si kwasababu ya pepo mbaya lakini inabidi kufikiri na kuona njia tofauti. Umesema tayari kuhusu msaada wa uganga kuna kazi yake katika shida kama haya kwenye nchi umepotoka. Kama kwa hali ya ndugu yako wanaongea sana akienda kwa daktari na wangepima hali, anahisi nini, anavyo sikia nini na anayo mawazo gani. Pia wanapima hali yake wakati onyo au mawazo yameanza na kipindi gani wamesumbua. Wanajaribu kujua hali yake na kutafuga kitu ambayo inaleta onyo. Kama inahitaji wanaweza kupima vipimo vya laboratorio au kufanya uchunguzi mengine ya uganga. Njia hii inawezekana kupata picha mzuri kuhusu shida. Kawaida mtu mwenye shida na nguvu sana inabidi aende kuona wafanyakazi wahodari mengi tu.

Pia inawezekana kwamba hali ya ndugu yako ni ya udaktari. Maana yake ni kwamba shida ni usumbufu ya ubongo. Onyo ambayo yeye amekuwa naye huweza kuwa na onyo ya kiusaikoloji. Maana ya hii ni kwamba jinsi mtu anavyo sikia hali ya kuwa kwa kweli imegeuka sana. Onyo inaweza kutokea wakati mtu anaamiki kitu ambayo si kitu cha kawaida, mawazo ya lazima, anasikia, anaona au anahisia mambo ambayo mtu wa kawaida katika hali moja hasikii, haoni, hahisi. Mtu anaweza kwa mfano kusikia sauti ambayo inaleta habari mfulani au kunusa harufu ambayo wengine hawanusi. Katika usumbufu ya usaikoloji mengine mtu anasikia kama watu wengine au kitu mfulani inasumbua au inatesa sana yeye. Shida ya usumbufu ya usaikoloji ni za aina mbali mbali. Maisha ya mtu na tabia ya mtu inafanya kwamba onyo gani atapata. Unaeleza kuhusu maisha ya ndugu yako na kwamba amekuwa na shida tangu mtoto mdogo. Hii ina hali anavyo sikia sikuhizi. Ujuzi magumu sana inaacha alama na inaweza kuleta hali wapi mtu anasikia kitu kinasonga sana. Wakati huo mtu anasikia hali ya kukaa kweli njia tofauti. Kitu amabayo inawasha hali ngumu inaweza kuwa kitu ambayo inakumbusha hali mbaya

Kama nchi yako kuna madaktari hodari ya usaikoloji itakuwa vizuri kama ndugu na familia wake wanaweza kuenda kuongea na hawa kuhusu shida. Shauri ambayo unaweza kumpa kwa wajamaa wako ni kwamba wanaeleza hali kwa wazi bila kuficha kitu ili daktari anaweza kukadiri hali.

Ni muhimu pia kwamba familia wako karibu na ndugu na wanasaidia ili wasiache yeye peke yake na shida wakati wowote. Hii inasaidia yeye kusonga mbele. Si shida kutumia tibu ya kijyeji mara moja na tibu ya daktari lakini ni muhimu kwamba hakuna kugombana wapi mganga wa kinyeji anakataa kutumia dawa ambayo daktari ameandika. Unaeleza lakini wapi tibu ya kinyeji hajaleta msaidizi kwahivyo itakuwa vizuri kutafuta utibabu tofauti.

Sirkku Suikkanen msaikoloji

Наверх


 

Яндекс.Метрика