Mpendwa msaikokoji, Ninakuuliza Wewe kuhusu kitu nimeona. Nilitembea njini wakati wa mchana na mtu alinisukuma na akapiga kelele sana kwa saiit. Yule mtu aliopiga kelele alikuwa mwanaume kijana na ananiogopesha. Tena ilionekana kwamba alikuwa amelewa. Niliogopa kusema kitu. Alipiga kelele kwasababu mimi nafanana tofauti kidogo kuliko Wafini. Kitu ambayo nilistuka sana ni kwamba ananishambulia. Kwa kweli ningebidi nisimamie vizuri kama mwanaume lakini sitaki kupigana. Naogopa kwamba nikiumiza mtu wananilaumu kwa ngumu kwasababu mimi ni mtu kutoka ngambo na sitaki kupata shida. Tena naogopa kwamba mimi kama mtu mwenye mgonjwa kidogo wananiweza kuumiza kwa nguvu paka nitakuwa kilema maisha nzima. Nimechoka sana tangu hii kitu kutokea na siwezi kutulia vizuri wakati natembea nje pekeyangu. Tena nasikia kama niko hofu kila wakati. Stress nasikia zaidi wakati natembea wakati wa kiza. Ni ngumu hata kutoka nyumbani kuenda dukani wakati wa kiza au kwa mfano kuenda kukimbia na kufanya mazoezi. Wakati huo inabidi kukuwa na hofu kila wakati. Tena kutembelea mjini haileti furaha kama zamani kwasababu nafikiri kwamba naweza kumkuta na yule mtu tena. Kwa aibu yangu nimepata kuona kwamba naogopa hata kivuli yangu kama wanasema. Hapa Finland nimeona pia jinsi watu wananiangalia sana kwa uonevu. Ni kawaida tu kwamba mtu ananiangalia sana na kwa macho kali sana. Pia nakuta watu ambayo wanasalimia kwa urafiki. Nafikiri lakini kwamba watu Wafini hawajui kufanya nini wakimkuta mtu ambayo anaonekana tofauti na kwamba watu wote ambayo wananifana kama mimi si wagaidi au shirika la Waislamu wakali. Nimekuwa na visura chache ya Wafini na wamelaumu kwamba watu wanatuchangaa wakati tunatembea pamoja. Tena kutumbua si ya urafiki. Mara nyingi nasikia kwamba napata huduma ambayo si kama ya Wafini wanapata. Kwa mfano tulikuwa benki na kisura changu. Wote tulifanya kitu moja; tulitaka kuweka amana ya kuingisha fedha kwenye akaunti za benki. Penki iliakikisha kila noti niliokupa na waliniuliza zilitokea wapi lakini hawakufanya vile kwa kisura changu. Hii nilisikia kama iliniumiza. Nimeishi Finland zaidi ya miaka kumi na naongea luga vizuri tu. Ni ngumu sana lakini kusikia kama kukuwa na uraya ya darasa la pili kwa njia moja au nyingine. Naamini kwamba hii mtazamo inatuleta sisi wahamiaji hasira kwasababu hakuna mtu alioweza kupokea kitu kama hii kila wakati. Tafadhali umpe shauri moja jisi ya ku pata nguvu, pata mawazo ya kufaulu kuendelea kuishi kwenye dunia wapi tuko. Lakaba ”Mwenye nywele mweusi”.

Wapendwa wa someaji na lakaba ”Mwenye nywele mweusi”, Mtazamo mwenye ubaguzi wa rangi ni ya kawaida tu kukiko tuko tayari kuamini. Hii inaonekana kwa njia ya kupiga kelele, njia ya jeuri, kutisha kama kutazama sana kama mtu amekasirika. Wahamiaji ambayo wako tofauti kuliko Wafini wanajua sana kuhusu hii jambo. Ni kawaida kwamba ni ngumu kwa mtu kusema kitu kama haya ambayo ni ya oga. Mtu hataki kuumiza watu Wafini na watu wanaongea kuhusu hii shida pamoja na marafiki tu pekee. Jinsi ya kutendea na ubaguzi ya rangi ambayo ni ya sawa au si sawa ni marufuku kabisa. Hata mtazamo ni marufuku pia na inavunja sheria ya Finland. Ni vizuri kukumbuka kwamba sheria inakataa hii kitu kabisa. Hapa kuna mwandishi kidogo kutoka Sheria ya umoja kwa wote 6§:” Katazo ya ubaguzi: Ni marufuku kupagua mtu kwasababu ya umri yake, uasili ya kitaifa, uraya, lugha, dini, itikaki, maono, afya, ukilema, jinsia au kitu kingine ambayo ni sababu ya mtu binafsi. Ubaguzi ya uonevu ya kijinsia kuhusu mwanamke na mwanaume imekatazwa katika sheria kuhusu usawa ya mtu. Maana ya ubaguzi ni: 1) mtu anasikia ubaguzi kwasababu mwingine anapata huduma tofauti kuliko mwingine wakati mantiki inawezekana kulinganisha (ubaguzi ya kabisa) ; 2) kwamba kuna sababu, kanuni au tabia ambayo inafanya kwamba mwingine ana kiwango mbaya wakati kulinganisha na wengine. Ni sawa lakiki wakati sheria, sababu au tabia iko na nia nzuri na wakati njia ni muhimu na kamili. (ubaguzi ambayo si ya moja kwa moja) ; 3) kuumiza au kutisha, dunisha, adhiri, shambulia thamani ya mtu au kikundi cha mtu (msukosuko) ; 4)maelezo au amri.” Kama jibu kwa ulizo yako: Mimi nafikiri kwamba hakuna njia moja jinsi ya kuzoea kuvumilia jinsi mbaya ya kutendea au hata kuweza kujikaza. Hakuna njia nyingine kuliko kufikiri kwamba ni jinai wakati imefikisha alama ya jinai. Sasa mara ya pili kitu ikitotea wakati unasikia mtu anakubagua au kuna ubaguzi wa rangi kumbuka mambo ma chache vizuri; kitu gani kilitokea, nani alifanya, wapi na lini. Baadaya ya hii uende kwa kituo cha afya cha hapa karibu au piga simu namba 112. Ni kazi ya polisi kufanya ripoti kuhusu kitu ambayo wewe unasikia ni jinai. Polisi anakuuliza wewe habari kuhusu kama kitu gani kilitokea, nani ndio mwenye kukosa na/au anafananaje, sehemu wapi jinai kilitokea kama anwani, kwa mfano jina la restaurant, umeumizwa kwa mfano ulienda kwa daktari na kama kuna hasama kwasababu ya nchi ulipotoka.

Polisi anakuita wewe tena kwa hoji mara nyingine. Wakati kuenda uchukue kitambulisho chako na fika wakati wa muda imepangiwa. Kama muda waliokupa si mzuri omba upate nyingine lakini wahi tu. Kwenye maulizo kuna wewe na polisi. Kama unahitaji mkalimani au mwanasheria wewe uko na haki ya kupata moja. Kama unauliza mkalimani kabla ya kuenda kwa hoji polisi anakuita mkalimani ambayo ni bure kwa wewe. Pia unaweza kuuliza mwanasheria afike pia. Uliza mwanasheria kama inabidi wewe ulipe mshahara wake. Soma vizuri mwandishi ya hoji ambayo polisi ameandika. Hakikisha kwamba kilakitu imeandikwa kamili. Kama kuna kosa omba warekebishe. Kama unafikiri jinai ni ya baguzi ya rangi hakikisha kwamba polisi anaandika ile kwenye ripoti. Wewe uko na haki ya kupata kopi kwa wewe pia. Kama mteswa/ mtu kwenye hoji anadanganya anavunja sheria pia. Kitu kile kinasumbua kazi ya polisi. Kama polisi hapati dalili ya kutosha kuonyesha kwamba ni jinai anaweza kuacha kufanya uchunguzi. Katika jinai ndogo polisi anaweza kupiga faini katika marudio. Mambo magumu polisi anapeleka kwa mshitaki. Mwenye mdai anaamua kama wanapeleka paka mahakamani. Katikoa jinai ndogo mshitaki halaumu kama ni jinai. Wakati mshitaki anatoa tuhuma inaweza kuchukua miezi kabla ya kuenda mahakamani.

Kama umeona jinai wewe ni shahidi. Changamsha mteswa aende kueleza jambo kwa polisi. Ni muhimu kwamba unaenda kwa polisi na kwa kafara kujiandikisha. Kama hufurahii kuhusu kazi ya polisi unaweza kuita mkurugenzi wa polisi alioshuhulika jambo. Eleza yeye kwamba umefanya kazi na nani na lini umekuwa katika kituo cha polisi. Unaweza kuandika mlalamko kwenye karatasi na kutuma mkuu wa polisi, halmashauri au wazara ya mambo ya ndani. Pia unaweza kufanya mlalamko kwa mtu wa kwenye mbunge wa Finland. Kazi yake ni kutunza haki za watu. Hapa Finland pia kuna mfanyakazi ambayo anaitwa vähemmistövaltuutettu. Kwenye ofisi yake kuna mapogezi wapi mtu anaweza kuenda kama amesikia au ameona ubaguzi kwasababu ya rangi ya ngozi au kwasababu unatoka ngambo. Pia unaweza kuenda pale kama umesikia ubaguzi ya rangi au hujapata huduma mzuri. Wakati wa kesi ya ubaguzi yule mfanyakazi anatoa hatua uliohitaji. Hali mengine si kazi yake lakini kuchunga na kutoa shauri wakati mtu amesikia ubaguzi kwasababu ya rangi ya ngozi au kwasababu mtu anatoea ngambo. Wakati mengine mfanyakazi anaweza kuongoza mteja kupata huduma kutoka ofisi nyingine. Kwa mfanyakazi aliochunga haki ya watu kutoka ngambo huweza kupiga simu: namba ya simu 071 878 8666. Muda wa kupokea simu ni siku ya kwanza (Jumatatu) paka siku ya tano (Ijumaa) saa 10-12. Yule mtu aliojibu kwenye simu hutoa shauri jinsi ya kuendelea na kuleta hatua nyingine ile jambo ishuhulike. Katika simu huduma inapatikana kwa lugha ya Kifini, Kiswidi na Kingereza. Katika wakati wa kujibu simu kunaweza kuwa na vipindi vya mkutano wakati hawajibu simu. Wakati huo simu inaweza kugeuka kwa mtu mwingine na yeye anasema muda wakati huduma inapatikana tena. Pia unaweza kuandika barua upesi au kutuma barua cha kawaida. Kama kuna hali ya ubaguzi au maswali mengine unaweza kutuma barua upesi kwa: ofm@ofm.fi. Mabarua inabiidi utume: Vähemmistövaltuutetun toimisto, Mikonkatu 25, PL 26, 00023 VALTIONEUVOSTO. Kama huelewi Kifini, Kiswidi au Kingereza unaweza kuandika barua au barua upesi kwa lugha yako pia na ofisi watatafsiri hii barua. Kuhusu hii hakuna malipo kwa mteja. Wanaomba lakini usiandike zaidi ya ukurasa mbili. Kama unataka kuenda kuwaona wafanyakazi mwenyewe inabidi kupanga muda. Huduma za mfanyakazi aliochunga haki ya watu ni bure pia.

Pia mengine kuliko jinai la kawaida ni jinai pia. Kwa mfano kwasabau ya rangi ya ngozi au kwasababu mtu ni kutoka ngambo na kuharibu heshima ya mtu na kutisha mtu kwa haramu. Mfano kutoka hapa ni kama mtu anaita mwenzake ”ryssä- Mrusi” au ”neekeri- mtu mweusi”. Kwa hivyo hata kama Finland kuna uhuru ya kusema ni marufuku katika sheria kuharibu heshima ya mtu, kuharibu heskima ya mtu kwa nguvu na kutisha mtu kwa haramu. Haya ni vitendo vya adhabu. Kuharibu heshima ya mtu inatokea wakati mtu analeta habari ambayo ni uongo au anadokeza kitu ambayo inaweza kuumiza, kuleta teso au dharau mtu. Kuharibu heshima ya mtu si kitu kama mtu anachambua mwingine kwasababu anafanya kazi kwa hadhara. Pia kwamba kuchambua mtu hapiti kiasi. Inawezekana kuharibu heshima ya mtu pia hata wakati mtu amefariki tayari. Kwa mfano kama kuleta habari ambayo si kweli au kudokeza kitu ambayo inaweza kuleta teso kwa mtu ambayo ni karibu na mfu. Katika kesi ya kuharibu heshima ya mtu inabidi mtu mwenyewe aulize polisi kufanya upelelezi. Kutisha mtu kwa haramu inatokea wakati kwa mfano mtu anaonyesha punduki kwa wenzake au anatisha kufanya jinai mfulani kwamba mtu anaogopa na anasikia usalama wake au mali yake kuna hatari. Pia kutisha kwa haramu ni jinai ya mtu mwenyewe, maana yake ni kwamba mteswa ya jinai inabidi yeye mwenyewe aite polisi.

Kama unasikia kwamba hali yako si sawa baadaya kitu cha kusukuma kutokea itakuwa vizuri kuongea kuhusu hali na daktari yako na kwa mfano kwa msaikoloji pia. Ni kawaida kwamba baadaya ya kitu kutokea mtu anasikia kama jambo inasonga sana na inaweza kuonekana kama uliviyo eleza mbele kuhusu kusikia kama nguvu ziko nyingi, kusikia hofu au msisimko. Mambo ambayo yana kumbusha kuhusu hali wakati uliumizwa yanaweza kuleta hali mbaya na mtu anaweza kwa mfano kulala vibaya au kwamba jambo inarudia kichwani hata wakati ukiwa macho. Mtu anaanza kuepuka pia sehemu fulani au mambo ambayo yanakumbusha kuhusu kitu ambacho kimewahi kutokea. Ni muhimu kupata msaada mapema wakati onyo inakusumbua. Katika hali fulani kafara ya jinai inaweza hitaji kuwa na fasirio kutoka daktari kwa ajili ya kizimba. Hii karatasi inaonyesha kilema ya mwili na pia teso ya kiroho.

Sirkku Suikkanen msaikoloji

Ofisi ya mfanyakazi mwenye wakilishi watu wadogo (vähemmistövaltuutettu, ombudsman for minorities) Mikonkatu 25, PL 26, 00023 Valtioneuvosto, Simu 071 878 8666. Muda wa mapogezi wa simu ni Siku ya kwanza (Jumatatu) paka Siku ya tano (Ijumaa) saa10-12 www.vahemmistovaltuutettu.fi kutoka internet unapata habari kwa malugha 13.

Msaidizi wa sheria inapatikana kutoka ofisi yake (oikeusaputoimisto).
Kila mji/ manispaa kuna ofisi ya kupata msaada kuhusu sheria.
Kupata habari yani wapi ofisi iko wapi hupata kujua kutoka:

- kitabu cha manamba cha simu
- kutoka mapogezi ya simu ya mji/ manispaa
- wizara ya haki (oikeusministeriö), simu  09-1601.
- kutoka internet: www.oikeus.fi/9361.htm

Habari zaidi inapatikana kwa mfano: www.rasmus.fi, baado hapa endelea sehemu: ohjeita rikoksen uhrille (maelezo kwa kafara ya jinai). Lugha inapatikana kwa Kikroatia, Kihispania, Kifaransa, kituruki,

Kitabu Haki kwa mteswa wa jinai ya ubaguzi wa rangi na uonovu: Kortteinen Juhani ja Makkonen Timo: Oikeutta rasismin ja syrjinnän uhreille, Ihmisoikeusliitto, Helsinki 2000


Siirry ylös


 

Яндекс.Метрика